May 27, 2016

Jicho Pevu: Zilazila La Westgate na Mohammed Ali

Jicho-pevu
Print Friendly

Hayawi hayawi hatimaye yamekuwa, zimekuwa siku nyingi za kubashiri, na siku nyingi za kunongonezana kuhusu kilichojiri wakati taifa lilitekwa nyara na magaidi kwa siku nne mtawalia.

Wakenya zaidi ya sitini walipoteza maisha yao katika jumba la Westgate lakini hadi sasa Wakenya hawajajua ukweli kuhusu yaliyojiri katika jumba la Westgate.

Je ni kweli kuna waliokuwa wametekwa nyara na magaidi na kuzuiliwa katika jumba hilo? Je ni kweli kuna magaidi waliouawa na wanajeshi?

Meza ya upekuzi ya Jicho Pevu na Inside Story usiku na mchana wamekuwa wakidurusu kila ukurasa na, kufanya mahojiano na kupitia hatua kwa hatua video za cctv kutoka jumba la Westgate na sasa wako tayari kukusimulia kilichojiri bila kuficha lolote.

Meza hii ilifanikiwa picha za pekee kuhusu matukio ya Westgate. Usiambiwe tena tizama makala haya yatakayokujia katika muda usiokuwa mrefu ukiwanaye mwanahabari mpekuzi mohammed ali.

Comments
6 Responses to “Jicho Pevu: Zilazila La Westgate na Mohammed Ali”
 1. Baba Mkenya says:

  KDF BURE KABISA. GOING THROUGH DEAD, INJURED PEOPLE TO LOOT SHAME ON THE GOVERNMENT OF KENYA TO DENY FACTS.

 2. Calvo Moe says:

  lol why does he talk like that ? talk normal Xa Mchanaaaaaaaaa lol

 3. Kinoti Kelvin says:

  not playiing

 4. Harriet Masai says:

  what a nation?

Leave A Comment